Huu ni mfumo wa kimtandao, ambayo umetengeneza mahususi kusaidia wafanya biashara wanaouza bidhaa kwa jumla na rejareja, kwa kuhifadhi taarifa na kuendesha biashara zao kwa urahisi na kisasa zaidi.
“Uza, Kopesha bidhaa kwa msaada wa MauzoSheet”
Kujiunga na huduma hii unahitaji kujisajili kwa kubonyeza kitufe cha JISAJILI hapo juu na timu yetu ipo tayari kukuhudumia. Kwa tatizo lolote au msaada wasiliana nasi kwa njia zetu za mawasiliano, ili kuanza kufurahia huduma zetu.
"Uza, Kopesha bidhaa kwa msaada wa MauzoSheet"
MauzoSheet inahifadhi kumbukumbu za mauzo yako yote na kukukokotolea bei kulingana na idadi ya bidhaa unazo uza/kopesha, faida, hasara na ukitaka itakuambia chenchi ya kumrudishia mteja.
Je, upo nyumbani, hotelini, shambani unakaguamazao yako au upo safarini kwenda kumsalimia bibi kijijini? MauzoSheet itakuambia nini kinaendelea dukani kwako, itakuambia Mteja akikopa, bidhaa gani inakaribia kuharibika (expire).
Unachotakiwa ni kuwa na kompyuta/Laptop au Simu iliyounganishwa na intaneti.
Tuna amini wafanyabiashara mbalimbali wanakumbana na changamoto za kuhifadhi kumbukumbu za mauzo, matumizi, madeni, faida, hasara, malipo ya wafanyakazi, taarifa za wateja na kadharika. MauzoSheet inawezesha mfanyabiashara kuhifadhi taarifa hizo na nyingine nyingi kwa urahisi zaidi.
Faidika kwa kua Wakala wa MauzoSheet.
Ukiwa kama Wakala wa MauzoSheet utafaidika kwa kupata gawio la asilimia ishirini (20%) ya makusanyo yote ya fedha yaliyo letwa na wateja uliowaunganisha kwenye huu mtandao wa kuendeshea biashara kisasa.
Unataka kutengeza fedha kijanja? Jiunge sasa na vijanawenzako kwenye MauzoSheet upige hatua kimaisha